MENU INAYOENDANA NA KAHAWA ILI UPUNGUE KWA HARAKA

Day 1

Asubuhi:
Ukiweza kuamka na kutembea au kukimbia polepole kwa muda wa dk.30 au hata kuruka kambani sawa
Baada ya hapo oga vizuri, kunywa kikombe kimoja cha Slimmim Coffee kwa kuichanganya kama nilivyoelekeza kwenye post ya chini hapo.

Kula matunda mengi sana kiasi chochote kile
Usile mkate wala mayai.

Mchana:
Kula kipande kimoja cha samaki cha kuchemsha kwa kuwekewa ndimu/ limao na chumvi tu. no more, no less……….kisiwe kikubwa sana.
Salad iambatane na samaki huyo pamoja na maji mengi sana ya kunywa.
Jitahidi kwa siku unywe hata glass 12 au zaidi kama utaweza.

Usiku:
Kula Salad/ mboga mboga na matunda meengi kadri tumbo litakavyotosheka.
Kunywa na maji halafu lala. Huo ndio mlo wako wa Day 1.

Day 2:
Asubuhi fanya kama ilivyokuwa day 1
Ila hapa unaweza kuongezea kula yai 1 na sausage 1 ya kuchemsha, usile mkate kabisa.
Matunda na maji kwa wingi

Mchana:
Vipande viwili vya kuku wa kuchemsha bila kuweka mafuta na ndizi moja ya kuchemsha(Bukoba) na mboga mboga za kutosha bila kusahau matunda.
Maji ndio ya msingi zaidi, kunywa kwa wingi sana.

Usiku:
Kunywa supu ya mboga mboga na matunda……baada ya hapo tunakutakia usiku mwema

Day 3:
Asub kama kawaida kikombe cha kahawa
Kwa siku hii unaweza kula kiazi kimoja kikubwa cha kuchemsha, na matunda na maji.

Mchana:
Kunywa bakuli moja kubwa la supu ya samaki au kuku, jitahidi sana usiweke mafuta ya aina yoyote katika supu hiyo na iskizidi robo kuku au kipande kimoja cha samaki ndani ya supu hiyo, usiweke ndizi wala kiazi.

Usiku:
Matunda na maji tu, halafu ulale salama

Day 4:
Asubuhi kama kawaida kikombe cha kahawa.
Baada ya kahawa unaweza kunywa glass moja ya fresh juice ya, water melon,machungwa au nanasi inafaa zaidi

Mchana:
Supu ya mboga mboga/ “Veg soup” na matunda kwa wingi yakiambatana na maji

Usiku:
Ndizi 2 za kuchemsha, mboga mboga na maji mengi tu

Day 5:
Asub kama kawaida kikombe cha kahawa
Matunda na maji kwa wingi

Mchana:
Samaki au Kuku wa kuchemsha na mboga za majani

Usiku:
Matunda na maji

Day 6:
Asub kikombe cha kahawa na yai moja la kuchemsha
Matunda na maji kwa wingi

Mchana
Supu ya mboga mboga weka kiazi au ndizi moja tu ndani ya supu.

Usiku:
Salad na matunda plus maji

Day 7:
Asub kikombe cha kahawa

Mchana:
Matunda, mboga mboga na kipande cha samaki au robo kuku vya kuchemsha

Usiku:
Matunda, mboga na fresh juice

Vitu vya kuzingatia katika mpangilio huu wa mlo:

Kama ni mnywaji wa Bia punguza sana au acha kabisa kunywa, ukishindwa kunywa 2-3 kwa siku.
Pombe kali si nzuri kwenye mpangilio huu.

Baada ya siku 7 unaweza ukapumzika siku 3 ukarudia kula kama kawaida ila usile chakula kingi wala chenye mafuta.

Unaweza kurudia mfumo huu si zaidi ya mara 3 mpaka utakapoweza kumudu kubadilisha mfumo wako wa kula mara kwa mara chakula kingi.

Hii haijatoka kwa daktari ni kwa majaribio yangu tu, atakae ona inafaa anakaribishwa. Ila sio vibaya mkapate ushauri wa mtaalamu kabla hamjaanza kufuata utaratibu huu.

Hayo ni mawazo tu kama kuna mtu ana mtazamo tofauti na bora zaidi ya huu tunakaribisha maoni ili tuweze ku share kama pana mapungufu pia wataalam wanaweza kuturekebisha. Ila Captain ilimsaidia kwa namna hii

Am not A Doctor

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s